MAUDHI MADOGO MADOGO AMBAYO HUWEZA KUMPATA MTU BAADA YA KUPATA CHANJO(COVID-19)

ELIMU KUHUSU CHANJO

• • • • •

MAUDHI MADOGO MADOGO AMBAYO HUWEZA KUMPATA MTU BAADA YA KUPATA CHANJO(COVID-19)


Kila chanjo ina Side effects au maudhi madogo madogo ambayo huweza kumpata mtu aliyechanjwa, Na tafiti zinaonyesha kwamba Maudhi haya madogo madogo huwapata sana Vijana kuliko watu wengine kutokana na Mfumo wa kinga zao za mwili kuwa juu zaidi.


Hata hivo sio lazima kila aliyepata chanjo kuanza kupata maudhi haya(side effects), kuna wengine hawapati kabsa, kuna wengine hupata kidogo sana n.k, vyote ni kulingana na mfumo na Uimara wa kinga ya mwili kwa Mtu husika


MAUDHI MADOGO MADOGO(SIDE EFFECTS) YA CHANJO YOYOTE ILE IKIWEMO YA COVID-19 NI PAMOJA NA;

 

 1. Maumivu, uwekundu au uvimbe sehemu ambapo ulichomwa chanjo


 2. Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na Homa baada ya kuchomwa chanjo


 3. Kupata Uchovu wa mwili baada ya kupata chanjo


 4. Kupata Maumivu ya kichwa


5. Kupata Maumivu ya misuli


6. Kuhisi Baridi sana mwilini


 7. Maumivu ya pamoja(sehemu mbali mbali za mwili)


 8. Kupata kichefuchefu na kutapika


9. Kuvimba kwa lymph Node


N.K

 

•Kwa asilimia kubwa maudhi mengi hutokea ndani ya siku tatu za kwanza baada ya chanjo na kawaida hudumu siku 1 hadi 2 tu.


- KUMBUKA; Kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari unapoenda maeneo ya kupata chanjo hii ya Uviko-19(COVID-19),


 Pia fahamu, kazi kubwa ya Chanjo yoyote ile ni kwa ajili ya kutoa KINGA dhidi ya Ugonjwa Flani na sio kwa ajili ya KUTIBU kama watu wengi wanavyochanganya.


CHANJO Haitibu bali inakinga...!!!!



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!