MSONGO WA MAWAZO
• • • • • • •
MSONGO WA MAWAZO HUSABABISHWA NA NINI?
Tatizo la msongo wa mawazo huweza kumpata mtu yoyote kulingana na hali anayopitia au mazingira aliyopo kwa wakati huo, katika makala hii tunachambua baadhi ya sababu au vyanzo vya kusababisha tatizo la msongo wa mawazo kwa watu, na dalili za mtu mwenye msongo wa mawazo.
✓ Je tatizo la msongo wa mawazo huweza kusababishwa na nini?
✓ Je utamjuaje mtu mwenye tatizo la msongo wa mawazo?
BAADHI YA SABABU KUU ZA KULETA TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO KWA WATU NI PAMOJA NA;
1. Mtu kupitia hali ngumu ya maisha ikiwemo kuwa na kipato kidogo sana au kuporomoka kiuchumi kwa gafla
2. Mtu kufukuzwa kazi au kusimamishwa kazi ambayo alikuwa anaitegemea kwenye maisha yake
3. Mwanafunzi kufeli mtihani,kudisco kwa wanachuo, au kufukuzwa shule kwa sababu mbali mbali kama vile; kubeba ujauzito wakati akiwa shuleni n.k
4. Matatizo kwenye mahusiano ya kimapenzi ikiwa ni pamoja na; kuachwa, kupigwa, kusalitiwa n.k
5. Matatizo na migogoro ndani ya ndoa
6. Kutokuelewana kati ya wanandugu wa karibu sana kwenye familia
7. Kubanwa na shughuli nyingi sana huweza kukuletea tatizo la msongo wa mawazo pia
8. Mama kuzaa mtoto mwenye matatizo kama vile magonjwa flani,udhaifu au ulemavu flani huweza kusababisha tatizo la msongo wa mawazo kwa mama na familia kwa ujumla
9. Kuwa na tabia ya kutamani vitu ambavyo huna uwezo navyo
10. Kutaka kila kitu kifanyike kwa usahihi unaotaka wewe bila kuwa na kasoro au makosa yoyote n.k
BAADHI YA DALILI ZA MTU MWENYE TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO
- Mtu kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu sana kuliko kawaida,mfano; mtu anaweza kufanya kazi ya kufagia chumba kimoja tu kwa zaidi ya masaa mawili
- Mtu Kuwa na tatizo la kukosa usingizi
- Mtu kuomba msamaha kila mara hata kwa vitu ambavyo kwa hali ya kawaida sio makosa
- Mtu kuanza kuongea mwenyewe
- Mtu kuwa na wasiwasi pamoja na hofu kubwa
- Mtu kukasirika kwa haraka zaidi kwa vitu vidogo sana,tabia ambayo hakuwa nayo hapo kabla
- Mtu kuhisi uchungu pamoja na kuonewa kila mara
- Mtu kujiona hawezi kufanya chochote
- Mtu kuanza kukaa peke yake na kusononeka muda wote,tabia ambayo hakuwa nayo hapo kabla
- Mtu kuanza kuongea maneno ya kukata tamaa ya maisha,kutaka kujidhuru au kujiua N.k
Mtu mwenye dalili kama hizi anahitaji msaada wa haraka zaidi ili asijepatwa na madhara makubwa zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!