Mtoto kukojoa kwa shida au kushindwa kukojoa

 MTOTO

• • • •

Mtoto kukojoa kwa shida au kushindwa kukojoa


Kwa namna moja au nyingine tatizo hili la mtoto kushindwa kukojoa au kupata shida sana wakati wa kukojoa huweza kutokea bila kujali umri wa mtoto wala jinsia yake.


HIZI HAPA CHINI NI BAADHI YA SABABU AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA UWEPO WA TATIZO HILO KWA MTOTO


1. Maambukizi ya magonjwa kwenye mfumo mzima wa mkojo yaani UTI n.k


2. Kuwepo kwa tatizo la kupata choo kigumu sana kwa mtoto yaani Constipation


3. Mtoto kupatwa na hofu kuu pamoja na wasi wasi kutokana na hali anayopitia kwa wakati huo pamoja na mazingira aliyopo


4. Matumizi ya vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha Caffeine mara kwa mara


5. Matatizo kwenye mfumo wa fahamu ikiwa ni pamoja na magonjwa(nerves diseases), Kuumia uti wa mgongo n.k


6. Kuwa na tatizo la kukuwa kwa tezi la Prostate


7. Upasuaji unaohusisha mfumo mzima wa mkojo


8. Matumizi ya baadhi ya Dawa


9. Kuwa na tatizo la mawe kwenye figo yaani Kidney stones


10. Kuwa na tatizo la Rectocele


11. Mrija wa mkojo kuwa mwembamba kuliko kawaida(Urethral stricture) au kuziba kabsa. N.k


Ni vigumu sana kugundua chanzo cha tatizo hili kwa mtoto wako kama huna utaalam huo,hivo ni muhimu sana kuongea na wataalam wa afya ili kujua chanzo cha shida hiyo pamoja na kupata vipimo na Tiba kwa mtoto wako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!