Mwanamke anayeanza mapenzi kwenye Umri mdogo yupo kwenye Hatari ya kupata Saratani ya Shingo ya kizazi
ELIMU YA AFYA
• • • • • •
Mwanamke anayeanza mapenzi kwenye Umri mdogo yupo kwenye Hatari ya kupata tatizo la Saratani ya Shingo ya kizazi
Mwanamke ambaye huanza kushiriki tendo la ndoa/ngono au mapenzi kwenye umri mdogo(chini ya miaka 18) yupo kwenye hatari kubwa ya kupatwa na tatizo la Saratani ya shingo ya kizazi.
Kama inavyofahamika,Saratani ya shingo ya kizazi au kwa kitaalam Cervical cancer husababishwa na kirusi aina ya HUMAN PAPILLOMA VIRUS(HPV).
Kirusi hiki huweza kuenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana.
HAYA NI MAKUNDI YA WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
1. Wanaonza mapenzi au kushiriki ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 18) kama nilivyokwisha kueleza hapo juu
2. Wenye wapenzi wengi au tunasema multiple sexual partners
3. Wanaofanya mapenzi bila kinga(ngono zembe)
4. Wanaofanya biashara ya Ngono
5. Wanawake wanaovuta Sigara
6. Wanawake wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi(HIV)
7. Wanawake wenye watoto wengi sana
8. Wanawake wanaotumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kama vidonge(Birth contraceptives pills) kwa muda mrefu sana,
mfano utumiaji wa vidonge vya majira au uzazi wa mpango kwa zaidi ya miaka mitano(5)
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!