TATIZO LA KICHWA CHA UUME KUWA CHEKUNDU,KUWASHA AU KUVIMBA

TATIZO LA KICHWA CHA UUME KUWA CHEKUNDU,KUWASHA AU KUVIMBA


Tatizo hili la kichwa cha uumwe kuwasha,kuvimba au kuwa chekundu kwa kitaalam hujulikana kama Balanitis.


Tatizo hili hutokea kwa asilimia 10% ya wanaume katika maisha yao, huku idadi kubwa ikiwa ni wale ambao hawajatahiriwa pamoja na wale wenye umri mdogo wa chini ya miaka 4. Japo pia hata wengine hupatwa na tatizo hili.


DALILI ZA TATIZO HILI


Tatizo hili huweza kuambatana na Dalili mbali mbali kama vile;


- Kupata maumivu


- Kichwa cha uume kuwasha sana


- Kichwa cha uume kubadilika rangi na kuwa chekundu


- Kichwa cha uume kuvimba


- Mara chache kupata maumivu wakati wa kukojoa kama vile mtu mwenye shida ya UTI


- Kupata vidonda kwenye kichwa cha uume


- Kutoa harufu mbaya kwenye uume


- Kutoa uchafu mweupe chini au kuzunguka ngozi ya uume

N.k


CHANZO CHA TATIZO HILI


Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa tatizo hili kama vile;


1. Mwanaume kutojisafisha vizuri sehemu za siri au uchafu(poor hygiene)


2. Mwanaume kutokutahiriwa


3. Kupata maambukizi ya fangasi sehemu za siri yaani Candidiasis or Genital Yeast Infection


4. Kupatwa na magonjwa mbali mbali ya Zinaa(STD's)


5. Kuwa na tatizo la Scabies


6. Kuwa na tatizo la Allergy ya vitu mbali mbali kama vile sabuni,mafuta,maji n.k


7. Kuwa na magonjwa mengine ya ngozi kama vile Psonosis au Eczema N.K


WANAUME AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


• Wanaume wachafu


• Wanaume ambao hawajatahiriwa


• Wanaume wenye tatizo la sukari, kwani kuongezeka kwa sukari kwenye ngozi huhamasisha bacteria pamoja na fangasi wazaliane kwa haraka na wafanye mashambulizi kwa kasi zaidi


• Wanaume wanene kupita kiasi


• Wanaume wanaopatwa na magonjwa ya zinaa mara kwa mara


• Wanaume wenye tatizo la allergy ya vitu mbali mbali

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!