TATIZO LA VARICOSE VEINS ( KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU) WAKATI WA UJA UZITO

AFYA YA UZAZI

• • • • •

TATIZO LA VARICOSE VEINS ( KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU) WAKATI WA UJA UZITO


Varicose Veins ni tatizo linalowapata baadhi ya wanawake wajawazito. Hili ni tatizo la kuvimba na kujikunja kwa baadhi mishipa ya damu hasa hasa kwenye maeneo ya miguu na mapaja. Pia linaweza kutokea kwenye maeneo ya njia ya haja kubwa na maeneo mengine.


CHANZO CHA TATIZO HILI LA VARICOSE VEINS


Mishipa ya Varicose kawaida husababishwa na kuwa na kuta dhaifu za mishipa na valves.  Ndani ya mishipa yako kuna vali ndogo za njia moja ambazo hufunguliwa ili kuruhusu damu kupita, na kisha kufunga ili kuizuia isirudi nyuma.  Wakati mwingine kuta za mishipa hukaza na kupoteza unyoofu, na kusababisha valves kudhoofika.



Hali hii hupelekea damu kusimama na kujikusanya sehemu moja ya mishipa na ndipo tatizo la kuvimba kwa mishipa huonekana.


MAMBO MUHIMU YA KUFANYA


- Ni vizuri kuongea na wamama na wadada katika ukoo au familia ili kujua kama hili tatizo liko katika familia yenu au la!


- Mama mjamzito inabidi ajitahidi kutokusimama kwa muda mrefu sana, Fanya mazoezi,tembea tembea na wala usisimame eneo moja kwa muda mrefu sana


 - Kuongezeka kwa msukumo wa damu au presha wakati wa ujauzito kunaweka stress kwenye mishipa ya damu,kitu ambacho huweza kuongeza uwezekano wa kutokea kwa tatizo hili


- kuongezeka kwa hormone aina ya Progesterone inalegeza misuli ambayo inaweza kusababisha kulegea kwa kuta,valves pamoja na kuvunjika kwa mishipa. 


Hata kama hukupata hili tatizo wakati wa ujauzito upo uwezekano wa kupata hemorrhoids au varicose veins baada ya kujifungua.


- Badala ya kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu, jaribu kukaa chini kwenye style ya kihindi yaani tailor sitting.(kama nilivyoelekeza kwenye mada ya mazoezi) Pia jaribu kuweka miguu kuelekea juu/elevated.


- Fanya zoezi aina la Pelvic rocking. Lala chini huku miguu ikiegemezwa juu ya kochi, kiti au kitanda huku magoti yamekunjwa. Relax katika position hii kwa dakika 10 hadi 15 halafu simama kisha piga piga miguu kwa mikono taratibu.


- Fanya mazoezi ya yoga ambayo yanafanya miguu ikae kwa juu, lakini hakikisha una mtaalamu wa kukufundisha jinsi ya kufanya haya mazoezi vizuri.


- Kuogelea na kutembea pia ni mazoezi mazuri yanayosaidia kukupa mzunguko mzuri wa damu. Unaweza pia kupata massage ya miguu kwa dakika tano kila siku. 


- Usivae nguo za kubana, viatu virefu, jizuie kukunja miguu ukikaa, na kukaa kwenye kiti au gari kwa muda mrefu hivi vitu huzuia mzunguko mzuri wa damu


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!