Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA KELOID,CHANZO PAMOJA NA DALILI ZAKE



UGONJWA WA KELOID,CHANZO PAMOJA NA DALILI ZAKE

Ugonjwa wa keloid huhusisha kuota nyama kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama vile sikioni n.k. Dalili za keloid zinaweza kujumuisha:

- eneo ambalo keloid hutokea huweza kuanza kwa kubadilika rangi na kuwa jekundu zaidi

 - Ngozi huanza kutanuka na kutuna,kisha nyama ya sehemu hiyo huanza kukua na kuongezeka ukubwa

- Kuna wakati makovu haya ya Keloid huweza kuwasha japo hakuna madhara yoyote ambayo huweza kutokea.

Mara nyingi ni vigumu sana kugundua wakati tatizo la keloid linaanza,mtu huanza kuona mabadiliko baada ya nyama kutokea sehemu husika kama vile masikioni n.k

CHANZO CHA TATIZO LA KELOID NI PAMOJA NA;

Uwepo wa majeraha mengi kwenye sehemu mbali mbali za mwili wako, hii ni pamoja na;

1. Kuwepo kwa makovu mbali mbali mwilini

2. Vidonda vinavyotokana na kuchomwa na kitu cha Ncha kali

3. Kutoboa Masikio

4. Makovu ya magonjwa kama vile tetekuwanga,chunusi na magonjwa ya ngozi

5. Kukatwa au kukwaruzwa na kitu cha ncha kali

6. Maeneo ambayo umefanyiwa upasuaji

7. Sehemu ambapo ulichomwa na sindano

N.k

 Inakadiriwa asilimia 10 ya watu hupata makovu ya keloid.  Wanaume na wanawake wana uwezekano sawa wa kuwa na makovu ya keloid.  Watu wenye rangi ya ngozi nyeusi wanakabiliwa zaidi na keloids.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments