LEUKEMIA
• • • • • •
UGONJWA WA SARATANI YA DAMU(LEUKEMIA),CHANZO,DALILI NA TIBA
Leukemia hii ni saratani ya damu ambayo huathiri na kushambulia zaidi tisu mbali mbali mwilini ambazo zinahusika na utengenezaji wa damu kama vile tissu za Bone marrow,Lymphatic system n.k.
CHANZO CHA SARATANI HII YA DAMU(LEUKEMIA)
- Hakuna sababu ya moja kwa moja iliyogundulika na kuonekana inasababisha aina hii ya kansa(kansa ya damu/Leukemia), japo kuna baadhi ya sababu ambazo huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo hili kama vile;
• Sababu za vinasaba vya tatizo hili katika familia au ukoo
• Kuwahi kupatwa na aina zingine za saratani au kansa kisha kupata huduma ya mionzi pamoja na baadhi ya dawa za kumsaidia mtu mwenye tatizo la saratani kwa muda flani
• Mtu kuwa na magonjwa mengine yanayohusisha damu
• Kupata miale mikali ya Mionzi n.k
• Uvutaji wa Sigara huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili
• Matumizi ya baadhi ya vitu vyenye kemikali kali n.k
DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA DAMU/LEUKEMIA
- Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa
- Mwili kuchoka kupita kiasi pamoja na kukosa nguvu
- Uzito wa mwili kupungua kwa kasi kubwa
- Mgonjwa kukosa hamu ya kula chakula kabsa
- Mgonjwa kuvimba ini,lymph nodes n.k.
- Kuwa na tatizo la damu kuvuja puani kwa kujirudia mara kwa mara
- Rahisi sana kwa mgonjwa kuvuja damu au kupata michubuko mbali mbali ya ngozi
- Ngozi kuwa na madoa doa ya rangi nyekundu kama vile maeneo ya usoni(tazama picha hapo chini) pamoja na maeneo mengine ya mwili
- Mwili kuvuja sana jasho kupita kiasi hasa wakati wa usiku
- Kupata maumivu makali ya mifupa n.k
MATIBABU YA UGONJWA WA SARATANI YA DAMU-Leukemia
• Yapo matibabu ya aina mbali mbali kulingana na ukubwa wa ugonjwa,chanzo chake pamoja na Stage uliopo. Ila kwa ufupi kuna Tiba mbali mbali kama vile;
✓ Tiba ya mionzi(Radiotherapy)
✓ Chemotherapy
✓ Bone marrow transplant
✓ Immunotherapy
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!