Fahamu kuhusu andropause, "ukomo wa uzazi kwa wanaume

Andropause, “ukomo wa uzazi kwa wanaume

Viwango vya chini vya testosterone vinaweza kutokea na kusababisha athari hususani katika afya ya ngono.

Maumbile ya kibaiolojia ya wanaume na wanawake huwa hayana mfumo unaofanana kila wakati. Mfano wa hili ni mabadiliko ya baadhi ya homoni za kawaida.

Kwa upande wa vitu kama vile homoni za estrojeni hatua kwa hatua huacha kuzalishwa katikati ya muongo wa tano wa maisha.

Kwa wakati huu, unaojulikana kama ukomo wa hedhi, mwanamke hupoteza uwezo wa kuzalisha mayai ya uzazi kutoka kwenye ovari na kupata hedhi na kuwa vigumu kupata mimba kwa njia za asili kwasabau hupoteza uwezo wa kuzalisha mayai ya uzazi.

Kwa upande mwingine kwa binadamu hakuna mchakato unaofanana. Homoni ya kiume inayohusishwa na uzalishaji wa mbegu za kiume (testosterone ) miongoni mwa kazi zake nyingine, huonekana kuendelea kubaki mara kwa mara katika maisha yote ya mwanamume , hata baada ya kufikia umri wa miaka 50, 60 au 70.

Ikiwa tunafuata hoja hii, neno “andropause” – ambalo limepata umaarufu kuelezea aina ya “kufikia ukomo wa uwezo wa kuzalisha wa wanaume”, na kupunguza uwezekano wa uzalishaji wa testosterone baada ya umri fulani – haina maana ya kimantiki, kulingana na wataalam.

Lakini ni muhimu kufikiria kuwa: kuna visa vinavyotokana na msururu wa matukio ambavyo huweza kusababisha kushuka kwa homoni za kiume testosterone na hivyo kusababisha athari mbaya ambazo hazikutarajiwa.

Hali hizi, zinazojulikana kama hypogonadism (ukomo wa uzazi wa kiume), zina vigezo vya uchunguzi na matibabu.

Hivi karibuni, miongozo ya usimamizi wa upungufu wa homoni za kiume imepitia mfululizo wa mabadiliko, kwa lengo la kuzuia matumizi ya kupita kiasi ya testosterone kama steroid ya anabolic, kwa madhumuni ya urembo kwa wanaume au wanawake

Hadithi ya andropause

“Maelezo yoyote ya andropause lazima yaanze na ukweli kwamba haipo,” anasema Dk Alexandre Hohl, rais wa zamani wa Jumuiya ya Brazil ya wataalamu wa magonjwa mbali mbali ya homoni (SBEm).

“Neno hili ni neologism lilibuniwa kutokana na dhana ya ukomo wa uzazi, asili yake ikiwa ni kutoka lugha ya Kilatini: linahusiana na usumbufu unaotokana na ukomo wa hedhi. Kwa maneno mengine, kumaliza hedhi ni kukomesha hedhi” , anaelezea.

“Kutoka hapo, mtu alikuwa na wazo la bahati mbaya la kuunda dhana ya andropause, ambalo linasababisha tu utambuzi wa makosa na matumizi yasiyo ya lazima ya testosterone,” analalamika Dk Hohl.

Daktari Luiz Otávio Torres, katibu mkuu wa Jumuiya ya madaktari wa maradhi ya kibofu cha mkojo ya Brazil, anakubaliana.

Dkt Hohl anaeleza kuwa katika maisha yao yote, wanaume hawana uzoefu wa jambo kama la kumaliza hedhi, kama wanawake wanavyofanya.

“Kibaiolojia , wanaume hupungukiwa kwa taratibu na uzalishaji wa homoni za kiume za kuzalisha testosterone, hasa baada ya umri wa miaka 40 au 50. Lakini kama ni mtu mzima mwenye afya, huenda akafikia miaka yake ya 60, 70 au hata 80 na viwango vya kutosha vya homoni hii, bila ya haja ya kuingilia kati au kuibadilisha,” anaelezea.

Upungufu huu wa taratibu na wa asili katika homoni ya kiume, ambayo huzalishwa na korodani, hutokea kwa kiwango cha asilimia 1.2 kwa mwaka kutoka umri wa miaka 40 au 45.

“Kwa maneno mengine, wanaume wanaweza hata kuwa na kupungua kwa testosterone, lakini hawaachi kuzalisha homoni kama wanawake,” Torres anaelezea kwa kifupi.

Lakini kushuka kwa homoni hii kunaweza kuongezeka kutokana na sababu nyingine , kama vile ugonjwa wa kisukari au kuongezeka kwa unene wa kupindukia wa mwili.

Kwa watu wenye magonjwa haya au mengine sugu, viwango vya testosterone vinaweza kupungua zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Hali hii inaitwa hypogonadism ya kiume.

Sababu nyingine zinazoweza kusababisha kupungua kwa homoni hii ni pamoja na magonjwa yanayoathiri tezi ya pituitary (muundo wa ubongo unaohusika na kudhibiti uzalishaji wa testosterone katika korodani) au viungo vya uzazi vya kiume vyenyewe.

Pia kuna watu ambao, kwa sababu za maumbile, hawapitii michakato inayohusiana na kubalehe na matokeo yake hawakupata ukuaji katika uume wao, korodani na nywele za siri.

Lakini je ni wakati gani madaktari wanashuku hypogonadism?

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!