Ticker

6/recent/ticker-posts

Koti la Michael Jackson lauzwa kwa £250,000 kwenye mnada



Koti la ngozi liliyovaliwa na Michael Jackson katika miaka ya 1980 limenunuliwa kwa £250,000 ($306,000).

Vazi hilo la rangi nyeusi na nyeupe, lililokuwa likivaliwa na mwimbaji huyo marehemu katika tangazo la Pepsi, lilitarajiwa kuuzwa kati ya pauni 200,000 na 400,000 katika mnada huo.

Koti hilo lilikuwa kati ya zaidi ya bidhaa 200 za kumbukumbu za muziki zilizouzwa London siku ya Ijumaa, ikiwa ni pamoja na koti la George Michael na kipande cha nywele cha Amy Winehouse.

Bidhaa zenye kuhusishwa na David Bowie, Oasis na The Beatles pia ziliuzwa mnadani.

Jackson alivaa koti hilo mnamo 1984, katika mfululizo wa kwanza wa matangazo ya biashara ambayo nyota huyo aliifanyia kampuni ya soda.

Matangazo hayo yanakumbukwa zaidi kwa tukio ambalo nywele za Jackson zilishika moto wakati wa kipindi cha upigaji picha, na kumwacha na majeraha mabaya.

Alikuwa amevaa koti tofauti wakati huo.



Post a Comment

0 Comments