kutokwa na uchafu ukeni kama maziwa mtindi
kutokwa na uchafu ukeni kama maziwa mtindi
JE KUTOKWA NA UCHAFU UKENI KAMA MAZIWA MTINDI NI TATIZO GANI?(swali la wanawake wengi,soma majibu hapa)
MAJIBU
Ni kweli kutokwa na uchafu ukeni kama maziwa mtindi ni kiashiria kikubwa kwamba kuna kitu hakipo sawa. Na mara nyingi uchafu huu huambatana na harufu au Miwasho katika sehemu za siri za Mwanamke.
Hiyo ni dalili ya tatizo la fangasi ukeni, ambapo kwa asilimia kubwa wanawake hushambuliwa na Fangasi jamii ya Candida Albicans, Fangasi hawa hupenda sana kushambulia maeneo ya sehemu za Siri.
Maambukizi ya fangasi (Yeast infection)
Maambukizi ya fangasi au kwa kitaalam “yeast infection” hutokea kutokana na ukuaji kupita kiasi(overgrowth)na ongezeko la fangasi wanaojulikana kama Candida albicans Ukeni.
Dalili za Maambukizi ya Fangasi Ukeni
Baada ya mwanamke kushambuliwa na fangasi hawa wa Candida albicans Ukeni, huweza kupata dalili mbali mbali ikiwemo;
1. Kutokwa na uchafu ukeni kama maziwa mtindi
2. Kupata miwasho Ukeni
3. Kuhisi hali ya kuungua eneo la ukeni n.k
NB: Hivo basi, endapo unatokwa na uchafu wenye rangi kama maziwa,na umeganda kama maziwa mtindi, na wakati mwingine huambatana na miwasho pamoja na harufu kali ukeni. Basi wewe una tatizo la Fangasi wa ukeni.
Kama una dalili hizo usikae kimya na kuteseka na shida hii,tuwasiliane ili upate msaada.
Matibabu ya kutokwa na uchafu ukeni kama maziwa mtindi
Baada ya kujua chanzo cha tatizo hili, Mwanamke ataanza kupewa tiba ikiwemo dawa jamii ya antifungal medications ili kutibu maambukizi ya Fangasi, Dawa hizi zipo katika mifumo mitatu ambayo ni;
- Za kudumbukiza ukeni kwa kitaalam (suppository),
- Za kupaka(cream),
- Au vidonge vya kunywa(pill).
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Rejea Vyanzo;
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!