Mashabiki wa Yanga wakinywa supu leo Jumapili Novemba 12 2023

Mashabiki nanwanachama wa Klabu ya Yanga wamejitokeza kwa wingi kunywa supu leo Jumapili Novemba 12 2023 katika ofisi za makao makuu ya klabu hiyo zilizopo Jangwani, Dar es Salaam kama walivyokuwa wametangaziwa.

Hafla hii inakuja baada ya kumkanda mtani wao Simba SC kwa bao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC Jumapili iliyopita katika Dimba la Mkapa na kuzawadiwa ng”ombe 10 ambao wameamua kuwachinja na kunywa supu.

Aidha Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amewanunulia chapati 5000 mashabiki wote waliojitokeza kunywa supu leo Jangwani.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!