Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amewataka Wasanii wanaovuta bangi na unga kujirekebisha na kuacha mara moja kwakuwa orodha ya wote wanaovuta anayo na kwamba Mamlaka hiyo inakamilisha ujenzi wa Maabara mpya ya Ukaguzi na Sayansi Jinai yenye mitambo ya kisasa na ikikamilika Wasanii hao watapimwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Akiongea leo November 14,2023 Jijini Dar es salaam, Lyimo amesema “Nitoe wito kwa Wasanii wanaotumia dawa za kulevya tuna orodha yao, tuna orodha ya wanaovuta bangi, tuna orodha ya wanaovuta heroin na cocaine, tunawapa muda wa kujirekebisha hii mitambo yetu ya maabara ikikamilika tutawachukulia hatua wote tutawapima na tukijiridhisha mnatumia mtachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa Mahakamani”
“Wafikishieni taarifa Wasanii tunawapa muda tu maabara ikikamilika tutashughulika nao, BASATA tulifanya kikao nao na waliridhia tuchukue hatua tutapeleka majina yao, hatutojali ukubwa wa Msanii, hatutotajli anapendwa vipi na Mashabiki ilimradi anatumia dawa za kulevya tutamchukulia hatua”
“Wasanii wengine wanashawishiwa na Wasanii wenzao kutumia bangi na dawa nyingine za kulevya, narudia tulikuwa hatujakamilisha ujenzi wa maabara yetu, maabara yetu ikikamilika tutawashughulikia”
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!