Ticker

6/recent/ticker-posts

Aina ya Mazoezi yanayosaidia kuongeza urefu wa kimo kwa Mtu



Aina ya Mazoezi yanayosaidia kuongeza urefu wa kimo kwa Mtu

Kuna msemo kuwa urefu watoka kwa Mola na upana wajitafutia mwenyewe. Aidha, kuna dhana kuwa mtu mfupi hawezi kufanya chochote kujiongezea urefu.

-Hii inatokana kuwa urefu wa kimo unategemea pakubwa Ulivyoratibiwa katika genes

-Hata hivyo, usikate tamaa kwa kuwa yafuatayo ni baadhi ya mazoezi yanayodaiwa kumsaidia mtu kuongeza kimo,

Mazoezi haya yananuia kunyoosha uti wa mgongo na viungo kama miguu na hivyo kuvifanya laini na rahisi kurefuka.

Tungetaka kuweka wazi kuwa hadi sasa, hakuna utafiti wa kisayansi wa kudhibitisha kuwa mazoezi haya yanamsaidia mtu kuongeza urefu wa kimo.

1. Kuning’inia kwenye chuma

Kuning’inia ni mojawapo ya tizi ambazo zinazodaiwa kusaidia uzani wa chini (kutoka kiuno kwenda chini) kurefusha misuli na mifupa.

Hii humsaidia mtu kuongeza urefu kwa nchi moja au mbili.

2. Mnyoosho wa Cobra

Mazoezi haya yananuia kunyoosha uti wako wa mgongo na hivyo kuufanya laini na mwepesi wa kurefuka.

Mazoezi haya ni muhimu katika kusaidia kukuza cartillage kati ya viungo na hivyo kusababisha kuongezeka kwa urefu.

Lala sakafuni uso wako ukitazama chini na viganja vyako vikiwa sakafuni chini ya mabega yako.

Kisha inua mgongo wako juu huku ukifanya kidevu chako kuangalia juu. Pinda mgongo uwezavyo,

Rudia hivi mara tatu au nne kwa muda wa sekunde 5 hadi 30 kila mara.

3. Kuruka kwa kutumia mguu mmoja

Hii ni mojawapo ya tizi nyepesi zaidi kwa kuwa unaweza kuifanya popote kokote na wakati unashughulika na shughuli nyingine kama kutazama TV.

Ruka kwa mguu wako wa kushoto mara nane huku ukielekeza mikono yake juu,

Kisha ruka na mguu wako wa kulia kwa njia hiyo hiyo.

Mazoezi haya ya kuruka yanadaiwa kusaidia katika kukuza ubongo, kuongezea nguvu za miguu na utengenezaji wa homoni za kuongeza kimo (growth hormones).

4. Kuogelea

Kuogelea kwa saa chache kwa siku tano kila wiki kunasadikika kuwa mazoezi mazuri ya kuongezea kimo au ukipenda urefu.

Kuogelea huhusisha viungo vingi vya mwili. Kuogelea humwezesha mtu kutumia miguu, mwili na mikono na hivyo kuongezea nguvu,

Mtindo wa ‘breast stroke’ unadaiwa kuwa mtindo unaosaidia pakubwa kuongezea urefu.

Hivyo, iwapo unataka kuongezea kimo, basi ni bora ujifunze kuogelea.

5. Kuruka kamba

Kuruka kamba kunadaiwa kusaidia pakubwa katika kuongeza kimo na hata urefu.

Hata hivo tafiti Zaidi za kisayansi zinahitajika ili kuthibitisha haya.!!

Via:Tuko



Post a Comment

0 Comments