Ajali yaua Trafiki wawili katika eneo la Soliwaya Wilayani Wanging’ombe

Askari wawili wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Njombe WP.7866 Coplo Elizabia Kizale (35) na Askari H.1027 Coplo Patrick Salehe (34) wamefariki kwa ajali ya gari katika eneo la Soliwaya Wilayani Wanging’ombe wakati wakielekea kazini jana December 04,2023.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Hassan Banga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika barabara kuu ya Makambako – Mbeya iliyohusisha gari ndogo aina ya Toyota Sienta No.T815 DXV baada ya kugongana na lori lenye namba za usajili IT Z.445 lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Zambia.

“Kwahiyo chanzo cha ajali hii ni gari ndogo kutokuchukua tahadhari wakati liki-overtake gari nyingine na kisha kwenda upande wa pili na wakati linakwenda pembeni likagongwa ubavu wa kushoto na ndani ya hiyo gari kulikuwa na askari Polisi”

Katika hatua nyingine Kamanda Banga amesema kumetokea pia ajali nyingine eneo la Igawilo Wilayani Njombe ambapo gari aina ya HOWO Semi trela No T .765 DNZ limegongana na gari ndogo Toyota VXR No T.602 EEC na kupelekea vifo vya Watu wawili na majeruhi wawili.

Amesema waliofariki kwenye ajali hiyo ni Luno Nyika (43) Mkazi wa Mbinga na Scolastika (35) ambaye ni Mtendaji wa Kijiji (VEO) Wilayani Mbinga ambapo wamefariki wakati wakipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe wakati wakipata matibabu.
Via #MillardAyoUPDATES

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!