Ticker

6/recent/ticker-posts

ATM maalum kwa ajili ya wananchi kujipima VVU wenyewe kwa hiyari



ILI kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI (VVU), Mkoa wa Mbeya umefunga ATM maalum kwa ajili ya wananchi kujipima VVU wenyewe kwa hiyari.

Mashine hizo ambazo zimeanza kufungwa kwenye maeneo ya kumbi za starehe lengo ni kupunguza maambukizi mapya kwa vijana.

Mradi huo wa mashine za ATM zinazotoa vipimo vya UKIMWI na kinga unatekelezwa na mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani PEPFA na kutekelezwa na shirika la HJFMRI katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa maambukizi ya UKIMWI kwa mujibu wa ripoti kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) iliyotolewa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa takwimu hizo za TACAIDS asilimia saba ya watu wazima Tanzania wenye umri wa miaka 15-49 wameambukizwa Virusi vya UKIMWI ambapo maambukizi kwa wanawake ni juu zaidi asilimia nane kuliko ya wanaume wenye asilimia sita.



Post a Comment

0 Comments