Mwanamke mmoja wa Uganda aitwaye Safiina Namukwaya mwenye umri wa miaka 70, amejifungua Watoto mapacha kupitia ujauzito alioupata kwenye matibabu ya kupandikiza (IVF) katika Kituo cha Kimataifa cha Hospitali ya Wanawake kilichopo Kampala, Uganda.
Taarifa ya kituo hicho ambacho kimesema Mwanamke huyo kwa sasa ndio anashikilia rekodi ya kuwa Mwanamke Mzee zaidi Afrika aliyejifungua hivi karibuni, imesema Mapacha hao wawili mmoja ni wa kiume na mwingine ni wa kike.
Kwenye mahojiano na NTV Uganda, Safiina amesema alipelekwa kwenye Hospitali hiyo na Rafiki yake ambaye naye alisaidiwa na kujifungua salama kwenye Hospitali hiyo “Sina maneno ya kushukuru kwa wema wa Daktari, kuna wakati nilisikia kuumwa sana kutokana na ujauzito wangu nikiwa nimemaliza karibu pesa zangu zote, nilimpigia Doctor Sali akanitafutia usafiri ulionileta hapa”
“Wanaume hawapendi kuambiwa kama umebeba Mtoto zaidi ya mmoja, toka nilipolazwa hapa Mwanaume wangu hajajitokeza lakini Dr. Sali amenisaidia katika kila kitu, Mume wangu alifariki 1992 na niliwahi kuharibikiwa ujauzito wakati wa ndoa, nilikua nawajali Watoto wa wenzangu nikawa najiuliza na mimi nitapata lini wangu wataonitunza uzeeni….”
Huu ni uzao wa pili kwa Safiina ndani ya miaka mitatu ambapo uzao wa kwanza ni wa Mtoto wake wa kike ambaye alijifungua akiwa na umri wa miaka 67 mwaka 2020.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!