Busu, kumbatio vyatajwa kuwa hatari kwa afya
Wananchi wametakiwa kuzingatia hatua za afya, ili kuepukana na maambuzi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo yale ya njia ya hewa na kuepuka vitendo vya kukumbatiana, kubusu, salamu za kushikana mikono, huku wakishauriwa kupata chanjo katika vituo vya afya.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui na kudai kuwa Hospitali za Unguja na Pemba zimepokea watu 15,310 kwaajili ya vipimo huku 198 wakikutwa na maambukizi ya magonjwa ya upumuaji na 29 walikutwa na virusi vya UVIKO-19.
Aidha, amesema, tangu Januari 2023 ndani ya Visiwa vya Zanzibar, jumla ya watu 37 wamefariki kutokana na UVIKO-19 na kuongeza kuwa uku akitahadharisha kuwa idadi ya watu wanaoripotiwa kukumbwa na changamoto ya upumuaji inaongezeka.
Ripoti za hivi karibuni zinaonesha ugonjwa wa Malaria na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa yanaenea kwa kasi na wananchi wamehimizws kuchukua tahadhari, licha ya Shirika la Afya Ulimwenguni -WHO kutangaza kudhibiti UVIKO-19 .
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!