Bwana na Bibi Wafariki kwa kupishana saa 23 tu.
Mamia ya Wananchi mjini Njombe wamejitokeza kwenye maziko ya pamoja ya Wanandoa waliofariki kwa kupishana saa 23 katika Mtaa wa Mjimwema,
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo shinikizo la damu (BP) lililomkuta Elizabeth Sawala (63) baada ya kifo cha Mume wake Inyasi Hongoli (71) kilichotokea asubuhi ya December 25, 2023 siku ya Christmas wakati akipelekwa Hospitali baada ya kudondoka nyumbani kwake.
Lenard Hongoli ni Mtoto wa tatu katika Familia hiyo ambapo ameiambia @AyoTV_ kuwa amekuwa akiwauguza Wazazi wake kwa miezi miwili lakini siku ya Christmas alipokuwa Kanisani ndipo alipopata simu ya jirani aliyemueleza kuwa Baba yake ana hali mbaya na akawahi nyumbani ili kumpeleka Hospitali ambapo wakiwa njiani kwenda Hospitali alifia miguu mwake.
“Tuliporudi nyumbani kwa ajili ya maombolezo Mama akapata presha ikabidi tumkimbize Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe na akalazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na aliporudishwa kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida tulienda kumuangalia tukaona anacheka akasema Watoto wangu wote njooni hapa akatuchapa makofi matatu kila mmoja kumbe ndio anatuaga maana baada ya muda Madaktari wakasema hali yake sio nzuri akimbizwe Hospitali ya Rufaa Mbeya lakini muda wa saa mbili alifia njiani maeneo ya Igulusi”
Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika ametoa wito kwa Wananchi kuwa na imani pamoja na uvumilivu kutokana na tukio hilo ambalo limeumiza Watu wengi kutokana na namna lilivyotokea huku Daktari wa tiba zitokanazo na mimea Titas Mabula akishauri kwa watu wanaojua wana presha kuhakikisha wanafuata njia za kitaalamu ikiwemo kupata muda mzuri wa kupumzika na kunywa maji ya vuguvugu angalau glass moja mara baada ya kupokea taarifa ya mshtuko.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!