Falun Gong: dhehebu lisiloruhusu watu kunywa dawa wakati wanaugua.
Wang na mkewe Chen wamekuwa wafuasi wa Falun Gong kwa zaidi ya muongo mmoja. Chen anasema, “Falun Gong ina miujiza.”
Anasema, “nilipata upele mwekundu katika mwili wangu wote, lakini upele ule uliondoka na uchungu ukapotea.” Chen anasema, “ninahisi Mwalimu Li ameutakasa mwili wangu. Ninamshukuru sana Mwalimu Li kwa kuponya ugonjwa wangu. Wagonjwa wengi, hata wenye saratani, wameponywa na Falun Gong.”
Lakini hakuna ushahidi huru juu ya madai hayo.
Chen anasema, “wanachama wa Falun Gong hawaugui. Mwalimu Lee alituambia ukiugua ni matokeo ya matendo yako. Huna haja ya kunywa dawa kwa kuugua.”
Chama cha Kikomunisti cha China kinasema mafundisho hayo ndiyo yanayofanya Falun Gong kuwa hatari. Lakini kundi la Falun Gong linasema serikali imeendesha kampeni ya propaganda ili kuharibu harakati zao.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!