Ticker

6/recent/ticker-posts

Janga la chakula linazidi kuwa baya "kwa kiwango cha kutisha," Sudan



Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva, Msemaji wa WFP Leni Kinzli amewaambia waandishi wa habari kwamba ingawa mgogoro huo haujapata “uangalizi wa kimataifa unaostahiki,” mzozo huo umewaweka wakazi wa Sudan kwenye ghasia, kuhama na kuteseka, na kuwaweka mamilioni katika hali mbaya zaidi wakati hali yao ilikuwa mbaya tayari.

Leni Kinzli ameelezea kuwa janga la chakula linazidi kuwa baya “kwa kiwango cha kutisha,” kama inavyooneshwa katika uchambuzi wa WFP uliochapishwa leo. “Uchambuzi umegundua viwango vya juu zaidi vya njaa kuwahi kurekodiwa katika msimu wa sasa wa mavuno, kwa kawaida kipindi ambacho chakula zaidi kinapatikana. “Ikiwa hakutakuwa na ongezeko kubwa la msaada wa chakula wakati wa msimu wa pungufu unapofika, maeneo ya wazi yanaweza kuona njaa mbaya ikiibuka, ambayo ni ya juu zaidi katika viwango.”

Vurugu zinaongezeka, uzalishaji wa kilimo unapungua

Naibu mwakilishi wa FAO nchini Sudan, Adam Yao amebainisha kuwa janga la chakula limechangiwa na kuongezeka kwa ghasia, uzalishaji mdogo wa kilimo, bei ya juu ya vyakula, matatizo ya tabianchi na watu kuyahama makazi yao.

Adam Yao amesema Sudan ina rasilimali za kutosha za ardhi na maji, mzozo unazuia wakulima kufanya kazi kwa kawaida kutokana na ukosefu wa usalama na ukosefu wa pembejeo za kilimo na kupanda kwa bei zao.

Kulingana na tathmini iliyofanywa na FAO, uzalishaji wa mazao makuu ya nafaka, ulezi na mtama, unatarajiwa kupungua kwa 24% na 50%, mtawalia, ikilinganishwa na msimu uliopita.

Kunyumbayumba kwa mvua na kuenea kwa wadudu pia kumechangia kushuka kwa uzalishaji, inaeleza FAO.



Post a Comment

0 Comments