Ticker

6/recent/ticker-posts

Kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois kukosa Euro 2024 kutokana na jeraha la Goti



Kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois kukosa Euro 2024 kutokana na jeraha la Goti.

Kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois amefichua kwamba atakosa kampeni ya Ubelgiji ya Euro 2024 kutokana na jeraha lake la goti mwezi Agosti,

Huko majira ya kiangazi, kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 aliondoka uwanjani akitokwa na machozi wakati uchunguzi wa MRI ulithibitisha kwamba ana shida ya Goti,

Wiki moja baadaye, alifanyiwa upasuaji chini ya usimamizi wa timu ya matibabu ya Real Madrid na akapata habari kwamba angekuwa nje kwa hekaheka nzima za mwaka 2023-24.

Sasa, mlinda mlango huyo wa Madrid amethibitisha kuwa jeraha hilo pia litamfanya akose kushiriki michuano ya Euro mwakani, ikiwa ni pigo kubwa kwa timu ya taifa ya Ubelgiji.

Alikiambia kituo cha Ubelgiji Sporza: ‘Kwa sababu ya jeraha, hata hivyo hakutakuwa na mashindano ya Ulaya kwangu,’ Courtois aliambia chombo cha Ubelgiji.

Nikibahatika, naweza kucheza mechi nyingine Mei. Lakini basi huwezi kuwa tayari kwa asilimia 100 kwa mashindano makubwa.’

Kwa kukosekana kwa Courtois, kocha wa Ubelgiji Domenico Tedesco ana Koen Casteels, Thomas Kaminski, Matz Sels, Arnaud Bodart kama chaguo la kulinda lango.



Post a Comment

0 Comments