Mabasi yaliyokuwa yamewabeba watoto wadogo zaidi ya 400 kutoka Zimbabwe yakamatwa Afrika Kusini
Maafisa wa mpakani nchini Afrika Kusini wanasema wamekamata makumi ya mabasi yaliyokuwa yamewabeba watoto wadogo zaidi ya 400 kutoka Zimbabwe bila wazazi au walezi wa kisheria katika operesheni ya kupambana na biashara haramu ya binadamu.
Maafisa hao wanasema watoto hao walikuwa “wanasafirishwa” hadi Afrika Kusini, ingawa shirika linalowakilisha raia wa kigeni wanaoishi Afrika Kusini linasema kuna uwezekano watoto hao walikuwa wakitumwa kuwatembelea wazazi wao wanaofanya kazi Afrika Kusini kwa likizo za mwisho wa mwaka. . Mabasi hayo yalirudishwa Zimbabwe.
Zaidi ya Wazimbabwe milioni 1 wanaishi Afrika Kusini, wengi wao kinyume cha sheria, wakiwa wamehamia jirani zao wa kusini katika kipindi cha miaka 15 ili kuepuka msukosuko wa kiuchumi wa Zimbabwe.
Kamishna wa Shirika la Kusimamia Mipaka la Afrika Kusini Mike Masiapato alisema Jumapili kwamba polisi wa Afrika Kusini walisimamisha na kupekua mabasi 42 yaliyokuwa yakiingia kutoka Zimbabwe Jumamosi usiku na kupata watoto 443 walio chini ya umri wa miaka 8 wakisafiri bila kusindikizwa.
“Tuliwanyima kuingia na kuwawezesha maofisa wa Zimbabwe kuwashughulikia kurudi Zimbabwe,” Masiapato alisema.
Mabasi hayo yaliruhusiwa kupitia upande wa Zimbabwe wa kituo cha mpakani cha Beitbridge, maafisa wa mpaka wa Afrika Kusini walisema.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!