Mama ajifungua watoto watano kwa wakati mmoja
Mwanamke mmoja amebarikiwa na watoto watano warembo ambao alijifungua kwa wakati mmoja na ameshiriki ushuhuda wake kwenye mitandao ya kijamii.
Katika video ya kufurahisha iliyoshirikiwa kwenye TikTok, mwanamke huyo aliyejitambulisha kama @ebyfullmoon alifichua kuwa aliwakaribisha wasichana wawili warembo na wavulana watatu.
Alionekana hospitalini alipokuwa akitembeatembea tayari kukaribisha malaika wake wachanga.
Tumbo lake lililochomoza lilivutia watu mtandaoni, ambao walimsifu kwa kuweza kulibeba kwa miezi tisa.
Alisema: “Nina shukrani na taadhima kuu moyoni mwangu kwako wewe Mungu wangu. Matokeo yalikuwa watoto watano, wavulana watatu na wasichana wawili warembo.”
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!