Nyota wa tenisi, Naomi Osaka anasema kujifungua ndio uchungu mbaya zaidi maishani mwake
Nyota wa tenisi, Naomi Osaka anasema kujifungua ndio uchungu mbaya zaidi maishani mwake huku akijiandaa kurudi kwenye tenisi kwa mara ya kwanza kama mama.
Nyota wa tenisi kutoka Japan, Naomi Osaka amefunguka kuhusu ugumu wa kujifungua na kuutaja kuwa uchungu mbaya zaidi maishani mwake.
Bingwa huyo mara nne wa Grand Slam anajiandaa kurejea kwenye tenisi ambapo alikuwa anasubiriwa kwa muda mrefu mwishoni mwa mwezi huu mjini Brisbane baada ya kukaa nje ya mchezo mwaka mmoja ili kujifungua mtoto wake wa kwanza.
Osaka, ambaye alimkaribisha duniani binti Shai akiwa na mpenzi wake rapa Cordae, miezi mitano iliyopita, atarejea katika hafla ya joto ya Australian Open kabla ya dimba mwezi Januari.
Akizungumzia uzoefu wake katika leba kwenye mahojiano na InStyle, Osaka alisema: ‘Nakumbuka nikihisi wakati huo, haya ndiyo maumivu mabaya zaidi maishani mwangu.’
‘Na ninajua kwamba ikiwa nitapitia hili, basi kila kitu kingine kitakuwa rahisi sana.’
Aliongeza: ‘Sidhani kama watu wanajua jinsi mimba ilivyo ngumu; hakuna mtu anayezungumza juu yake sana.
Kuingia ndani yake, unafikiri: “Oh, ni safari hii nzuri.” Lakini ni mbaya pia.’
Osaka anakiri katika mahojiano kwamba awali alikuwa na wasiwasi juu ya kama angekuwa mama mzuri wa Shai,
Mwanadada huyo amekuwa na Cordae tangu 2019, lakini baada ya kujifungua Shai wanandoa hao walizua hofu kwamba walikuwa wametengana miezi michache tu katika safari yao kama wazazi.
Osaka amezima uvumi huo, hata hivyo, baada ya kufichua kuhusu uhusiano wao: ‘Tulijenga msingi mzuri sana. Sijui ni kwa sababu ni mtu mpole tu, lakini nadhani tunaheshimiana. Na ikiwa hatukubaliani katika jambo fulani, tunalizungumza.
‘Mwisho wa siku, sote tunataka kilicho bora kwa Shai.’
‘Yeye ni msafi sana,’ alisema kuhusu binti yake wa miezi mitano. ‘Kama, kila wakati ananiona, bila kujali, atatabasamu”.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!