PICHA: Mbarouk akisaini kitabu cha maombolezo kwenye Ubalozi wa Kuwait

PICHA: Mbarouk akisaini kitabu cha maombolezo kwenye Ubalozi wa Kuwait

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, amesaini kitabu cha maombolezo kwenye Ubalozi wa Kuwait jijini Dar es Salaam kutokana na  kifo cha Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah.

Kiongozi huyo alifariki Desemba 16,2023  akiwa na umri wa miaka 86 ambapo aliongoza taifa hilo kwa miaka mitatu iliyopita.

Balozi Mbarouk ametoa salamu za pole za Serikali ya Tanzania kwa Balozi wa Kuwait nchini,  Mubarak Mohammed Alsehaijan na amemuelezea  Hayati Sheikh Nawaf al-Ahmad kuwa atakumbukwa daima kama mwanadiplomasia na kiongozi imara aliyejitolea maisha yake katika masuala ya amani.

“Kiongozi huyo atakumbukwa kama kiongozi mahiri wa Kuwait aliyeimarisha ushirikiano wa karibu kati ya Kuwait na Tanzania.

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunapenda kutoa salamu zetu za pole kwa wananchi wa Kuwait kwa kuondokewa na kiongozi bora na mpenda amani. Roho yake Ipumzike mahali pema peponi,” ameongeza  Balozi Mbarouk

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!