Serikali ya Israel yaijulisha Tanzania kuwa Mtanzania Joshua Mollel aliuawa na Hamas

Serikali ya Israel yaijulisha Tanzania kuwa Mtanzania Joshua Mollel aliuawa na Hamas.

Serikali ya Israel imeijulisha Tanzania kuwa Mtanzania Joshua Mollel aliyekuwa anasoma nchini Israel aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la Hamas 7 Oktoba 2023.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ambapo ameeleza kuwa

“kwa sasa Serikali inaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel, kuungana na Balozi wetu na maafisa waliopo huko,

kukutana na kuzungumza na mamlaka za nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada.” Ameandika Waziri katika mitandao ya kijamii.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!