TMA yatoa Tahadhari! Mvua kubwa kunyesha mikoa 7.
Baadhi ya maeneo katika mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro na Mtwara yanatarajia kupata mvua juu ya kiwango kwa siku mbili kuanzia leo Desemba 1, 2023, hivyo wakazi wa maeneo hayo wameombwa kuchukua tahadhari.
Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya utabiri wa hali ya hewa wa siku tano zijazo kuanzia Novemba 30, 2023 uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa vyombo vya habari.
Taarifa hiyo iliyotolewa Novemba 30, 2023 inaeleza kuwa, mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma inatarajiwa kupata mvua hiyo, Desemba Mosi.
Huku siku siku inayofuata, mikoa ya Morogoro, Ruvuma na Mtwara nayo inatarajiwa kupata mvua hizo.
“Mvua hii itasababisha baadhi ya makazi kuzungukwa na maji na kuathiri baadhi ya shughuli za kiuchumi.
TMA imekuwa ikitoa taarifa kila wakati kwa wananchi kuhakikisha hatua muhimu zinafuatwa ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!