Tunahitaji kujiandaa dhidi ya janga jingine la ugonjwa: António Guterres

Tunahitaji kujiandaa dhidi ya janga jingine la ugonjwa: António Guterres

Wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga, daktari mwanamke anayeongoza kundi la wataalamu wa afya wanaojitolea kuhudumia wagonjwa wa COVID-19 na wanaochunguzwa katika hospitali ya jamii Ufilipino.

Janga la ugonjwa lijalo litakapotokea ni lazima tuchukue hatua kwa ufanisi zaidi kwa kuandaa na kujumuisha mafunzo tuliyojifunza kutokana na janga la COVID-19, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya kimataifa ya kukabili milipuko ya magonjwa ambayo huadhimishwa kila Novemba 27 kama leo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anabainisha kuwa janga la COVID-19 sio tena dharura ya kiafya ya kimataifa, lakini ugonjwa huo bado unazunguka, na athari zake mbaya bado zinaendelea kuhisiwa.

Kwa mujibu wake Bwana Guterres, uharibifu wa kiuchumi unaosababishwa na janga hilo bado haujaondolewa, na mifumo ya afya ya nchi nyingi inakabiliwa na shida kubwa. Zaidi ya hayo, mamilioni ya watoto wako katika hatari ya kuwa wagonjwa kwa kukosa chanjo za kawaida za utotoni. Miaka mitatu baada ya chanjo ya kwanza ya COVID-19 kutengenezwa, mabilioni ya watu bado hawajalindwa – idadi kubwa katika nchi zinazoendelea.

Kuimarisha mifumo

“Kwa kufanya kazi pamoja, dunia lazima iboreshe uchunguzi wa virusi, kuimarisha mifumo ya afya na kutimiza ahadi ya chanjo ya afya kwa wote,” Guterres anahimiza. “Lazima tuondoe uwezekano wa maafa ya kimaadili na kiafya wakati nchi tajiri zinaweka akiba na kudhibiti vifaa tiba ili kupambana na milipuko ya magonjwa, na kuhakikisha kila mtu anapata uchunguzi, matibabu na chanjo.” Katika muktadha huu, kiongozi huyu wa Umoja wa Mataifa anatoa wito wa kuimarishwa kwa mamlaka na kuongeza ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani.

Guterres ana imani kuwa juhudi hizi zinazaa matunda. Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Kuzuia Majanga ya Magonjwa, Maandalizi na Hatua mnamo Septemba mwaka huu ulitoa tamko la kisiasa la dhati. Hii inakamilisha mazungumzo ya mkataba wa majanga ya magonjwa huko Geneva.

Usawa

Katibu Mkuu Guterres anapendekeza kuwa nchi zijitahidi kuendeleza makubaliano ya kina yenye kulenga usawa na Baraza la Afya la Ulimwengu, ambalo litafanyika Mei mwaka ujao 2024.

“Sote tuzingatie masomo ya janga la COVID-19, tujitayarishe na kujenga ulimwengu mzuri na wenye afya kwa wote,” Guterres amehitimisha ujumbe wake.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!