Wanaolewesha Wanawake Dar Wadakwa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia operesheni maalum iliyoanza mwezi September, 2023 na inayo endelea katika maeneo mbalimbali Jijini,

limewakamata Watuhumiwa mbalimbali wakiwemo Watu wawili (majina yamehifadhiwa kwa sababu za uchunguzi) ambao huwatongoza Wanawake na kuwawekea dawa za kuwalewesha, kisha kuwafanyia udhalilishaji wa kingono ikiwemo kuwapiga picha.

Kamanda wa Kanda Maalum Muliro Jumanne amesema Watu hao pia huiba simu, laptop na fedha za Wanawake hao na kutishia kuwaua iwapo watasema chochote kinachohusu uhalifu huo.

Watuhumiwa hao wamekamatwa na vitu mbalimbali walivyoiba ikiwa ni pamoja na laptop 10, simu za mkononi za aina mbalimbali zipatazo 305, Televisheni 36, kamera 4, subwoofer 3 na makava ya simu 160 ambapo vitu 33 kati ya vyote vilivyokamatwa tayari vimetambuliwa na Wamiliki wake.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!