Watoto wengi hulemea upande wa Mama ndio maana akina Baba wengi wanakufa mapema
Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda amewashauri Wazazi wa kiume kujenga tabia ya kuwa karibu na Watoto wao ili baadaye wakizeeka wawasaidie badala ya kuwasaidia Wazazi wa kike pekee huku akiwataka pale wanapotoa fedha za matumizi kwa Wake zao watoe wakati Watoto wakiwepo.
Amesema hali hiyo itasaidia Watoto kujua kuwa fedha za mahitaji yao zinatolewa na Baba zao tofauti na wanapotoa kwa siri kwani inasababisha Watoto kuamini kuwa wanahudumiwa na Mama zao.
RAS Seneda ametoa ushauri huo leo Jumatano December 13, 2023 wakati akiongea na Watumishi wa Umma wa Tarafa ya Songwe ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za Watumishi wa Wilaya ya Songwe ambapo amesema “Tafuteni hela kihalali usiibe hela zetu (za Serikali) za miradi, ukipata hela kumbuka Wazazi wako usiwasahau na mkiwasaidia Wazazi wasaidieni kwa usawa kuna tabia ya watu kuwasaidia Wamama tu, unajua Wababa wanakwama eneo moja kwa sababu ya ubize kazi yao ni kuwasogezea Wamama wapeleke hela”
“Wakati mwingine toa ile hela Watoto wakiwepo, ile hela ya ada ile unaihesabu hapo wanaona, hela ya matumizi unatoa na wao wakiwepo ili wakimaliza wajue kuwa kumbe Mama mbwembwe zake zote ni Baba, Watoto wengi wanaishia kuelemea upande wa akina Mama ndio maana akina Baba wengi wanakufa mapema, Wababa wanajitoa sana lakini nao wanafeli katika kutengeneza bond kwa Watoto wao” ——— Happyness.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!