Watu wenye tatizo la hypochondriamu kuwa kwenye hatari ya kufa mapema Zaidi
Watu wenye tatizo la hypochondriamu kuwa kwenye hatari ya kufa mapema Zaidi.
Utafiti mpya wa watu ambao waligunduliwa na tatizo la hypochondriamu(hypochondria) uligundua kuwa walikuwa na hatari ya asilimia 84% ya kuongezeka kwa vifo vya mapema na waliishi chini ya miaka 5 kuliko watu wasio na ugonjwa huo(karibu miaka 5 ya kuishi kupunguzwa).
“A new study of people who were diagnosed with hypochondria found that they had an 84% increased risk of early death and lived about 5 fewer years than people without the disorder”.
Tatizo la hypochondria kwa jina lingine hujulikana kama “illness anxiety disorder”,
Wataalam wa afya walitazama tatizo hili kama tatizo la afya ya akili yaani psychiatric condition.
Moja ya Dalili zake kubwa ni Mtu kuwa na wasiwasi kupita kiasi hadi kufikia hatua ya kuugua,
Dalili kuu ni wasiwasi mwingi juu ya kuwa mgonjwa sana. Dalili zingine ni pamoja na kuwa na wasiwasi kwamba hisia za kawaida za mwili – kama vile tumbo kunguruma au kuwa na kelele au muwasho mdogo wa ngozi – ni ishara za ugonjwa mbaya.
Kwa Utafiti huu, Watafiti walichambua takwimu za watu Zaidi ya 4,000 wanaoishi nchini Sweden ambao tayari waligundulika kuwa na ugonjwa huu”illness anxiety disorder” kati ya Mwaka 1997 na 2020.
Watafiti walilinganisha watu wenye Ugonjwa huu na wale wasio na ugonjwa huu lakini wenye taarifa za kufanana kama vile; Umri pamoja na Jinsia, Na pia wanaoishi kwenye nchi hiyo hiyo Moja.
Matokeo ya Utafiti yamechapishwa mwezi huu kwenye Jarida la “JAMA Psychiatry” na yameonyesha kuwa;
Watu wenye tatizo la hypochondria wana uwezekano mkubwa wa kufa mapema kwa Sababu zinazofahamika na zisizofahamika(natural or unnatural causes).
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!