Asilimia 12 ya wajawazito walifanyiwa upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni 2023
Asilimia 12 ya wajawazito walifanyiwa upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni 2023
Na. WAF – Dar es Salaam
Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza vituo vya Afya vinavyofanya upasuaji wa dharura 523 imesaidia wanawake 226,187 sawa na asilimia 12 kufanyiwa upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni Mwaka 2023.
Waziri Ummy amesema hayo Januari 10, 2024 wakati akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za Afya nchini kwa mwaka 2023 wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es salaam.
Waziri Ummy amesema Mwaka 2022 vituo vya Afya vyenye uwezo wa kufanya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni vilikuwa 340 vikaongezwa vituo 48 Mwaka 2023 jumla vikawa vituo 388 vya Afya vinavyofanya upasuaji wa dharura, lengo ni kuhakikisha asilimia 50 ya Vituo vya Afya nchini vinatoa hudma za CEMONC.
“ongezeko la vituo vya kufanya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni vimewezesha kuokoa Maisha ya wanawazito na vichanga vyao, mfano Kituo cha Afya Kitunda (Tabora) kilikuwa takribani kilometa 160 kutoka Hospitali ya Wilaya ya Sikonge na hivyo wamama wengi walikuwa wanapoteza Maisha wakiwa wanasafirishwa kwenda Hospitali ya Wilaya.” Amesema Waziri Ummy
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!