Burundi imesema imefunga mpaka wake na Rwanda, ikiwa ni wiki mbili sasa baada ya kulituhumu taifa hilo jirani kuwaunga mkono waasi waliofanya mashambulizi nchini humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi Martin Niteretse amesema uamuzi huo umeafikiwa baada ya kubaini kuwa, Rwanda inawahifadhi wahalifu wanaowashambulia Warundi. Madai ambayo Kigali imekuwa ikiyakanusha.
Kundi la RED-Tabara linashtumiwa kuendesha mashambulizi makali katika taifa hilo la Afrika Mashariki.Tangu 2015 kundi hilo halikuwa likifanya mashambulizi lakini tangu Septemba 2021, limekuwa likifanya mashambulizi kadhaa, ikiwa ni pamoja na dhidi ya uwanja wa ndege wa jiji kuu la Bujumbura.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!