Dalili za nimonia kwa mtoto, Fahamu hapa

Dalili za nimonia kwa mtoto, Fahamu hapa

Nimonia(Pneumonia) ni maambukizi ya mapafu ambayo husababishwa na virusi au bakteria, Vijidudu hivi hufanya vifuko vya hewa kwenye mapafu kujazwa na majimaji (kohozi au ute). Hii inafanya kuwa vigumu kupumua na kusababisha mtoto wako kukohoa.

Fahamu: Nimonia huua watoto zaidi kuliko ugonjwa mwingine wowote wa kuambukiza.

Ingawa hata watu wazima huweza kupata ugonjwa wa nimonia, ugonjwa huu hushambulia na kuua Watoto Zaidi ulimwenguni kote.

Kila mwaka, Nimonia inaondoa maisha ya zaidi ya watoto 725,000 walio chini ya umri wa miaka 5, ikiwa ni pamoja na karibu watoto wachanga 190,000, ambao wako katika hatari ya kuambukizwa.

Kila siku, angalau Mtoto mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa Nimonia kwa kila sekunde 43, na Karibu Vifo vyote vinaweza kuzuilika.

Ni jambo lisilo na udhuru kwamba maelfu ya watoto hawawezi kupata huduma muhimu za afya na matibabu, ambayo yanaweza kuzuia nimonia na kuokoa maisha yao.

Chanzo cha ugonjwa wa Nimonia(pneumona)?

Nimonia ni maambukizi ya mfumo wa kupumua ambayo huathiri mapafu. Maambukizi haya hayana sababu moja – yanaweza kutokana na maambukizi ya vimelea kama vile;

  • bakteria,
  • virusi
  • au fungi

Wakati mtoto ameambukizwa, mapafu yake yanajaa maji na inakuwa vigumu kupumua. Watoto ambao kinga zao hazijakomaa (yaani watoto wachanga) au dhaifu – kama vile wenye utapiamlo, au magonjwa kama VVU – wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa ugonjwa wa nimonia.

Dalili za nimonia kwa mtoto

Fahamu hapa kuhusu dalili za ugonjwa wa pneumonia;

Kwa vile nimonia ni maambukizi ya mapafu, dalili za kawaida ni;

  • kukohoa,
  • kupumua kwa shida
  • na homa.
  • Watoto walio na nimonia kwa kawaida hupumua haraka, au kifua chao kinaweza kuvuta au kujirudisha nyuma wakati wa kuvuta pumzi (kwa mtu mwenye afya njema, kifua hupanuka wakati wa kuvuta pumzi).

– Kupumua haraka na kwa shida

– Kupata homa

– mwili kutetemeka sana

– Kupata maumivu ya misuli ya mwili

– Kukosa hamu ya kula chakula au kunyonya

– Kukohoa

– Kupata maumivu ya kifua

– Kupata Uchovu sana wa mwili

– Mwili kuwa Dhaifu sana

– Kupata kichefuchefu na kutapika n.k

Nimonia inayosababishwa na virusi mara nyingi sio kali kuliko inayosababishwa na bakteria. Dalili kwa kawaida huanza kama mafua. Na zinazidi kuwa mbaya zaidi kwa siku chache.

Nimonia inayosababishwa na bakteria inaweza kuja ghafla na homa kali, kupumua haraka na kukohoa.

Aina zote mbili za pneumonia zinaweza kusababisha kikohozi kwa mtoto kwa wiki kadhaa baada ya homa kukoma.

Nimonia inasambaa Je?

Nimonia inaambukiza na inaweza kuenea kupitia chembechembe zinazopeperuka hewani  kupitia (kikohozi au kupiga chafya). Inaweza pia kusambazwa kupitia vimiminika vingine, kama vile damu wakati wa kujifungua, au kutoka kwenye sehemu zilizochafuliwa.

Jinsi gani Nimonia hugundulika kwa mtoto?

Njia ambazo ugonjwa wa Nimonia huweza kugundulika kwa mtoto ni pamoja na;

  •  physical exam, ikiwa ni pamoja na kuangalia mifumo isiyo ya kawaida ya kupumua na kusikiliza mapafu ya mtoto.
  • chest x-rays
  • Au vipimo vya damu(blood tests)

Matibabu ya Ugonjwa wa Nimonia)pneumonia)

Matibabu ya nimonia inategemea na aina ya nimonia. Katika nchi zinazoendelea, idadi kubwa ya matukio ya nimonia husababishwa na bakteria na inaweza kutibiwa na antibiotics za gharama nafuu.

Hata hivyo watoto wengi wenye nimonia hawapati dawa za kuua vijasumu wanazohitaji kwa sababu wanakosa huduma bora za afya. Sababu nyingine za nimonia ni virusi au mycobacteria (k.m. zile zinazosababisha kifua kikuu) zinazohitaji matibabu mengine. Kifua kikuu haswa mara nyingi hubaki bila kutambuliwa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!