Ticker

6/recent/ticker-posts

Dawa ya gono kwa mwanaume



Dawa ya gono kwa mwanaume

Je, ni ipi dawa sahihi ya kutibu ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea)?

Dawa ya gono kwa Mwanaume; Baada ya kupata Maswali mengi kuhusu dawa sahihi ya Gono kwa Mwanaume,tumeambua kukuandalia Makala hii hapa;

Kisonono ni ugonjwa wa Zinaa ambao husabababishwa na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama Neisseria gonorrhoeae,

Ugonjwa huu wa kisonono ndyo hujulikana kama Gonorrhea au kwa kifupi wengi hupenda kuita “Gono”, Soma Zaidi hapa;

Dawa ya gono kwa mwanaume huweza kutibu kabsa tatizo hili ikiwa umepata tiba Sahihi,

Ni muhimu sana kupata Maelekezo kamili kutoka kwa Wataalam wa afya Wakati unapata au Kutumia Dawa ya Gono kwani badala ya kutibu gono unaweza kusababisha tatizo lingine linalojulikana kama “Usugu wa Dawa” ambapo vimelea hivi vya bacteria hutengeneza usugu kwenye dawa-Antimicrobial resistance”

Kwa hivi Sasa,Ukinzani wa viua vijidudu kwenye ugonjwa wa kisonono unazidi Kuongezeka, Hali ambayo hupelekea dawa ya Kutibu kwa mafanikio ugonjwa wa Gono au kisonono Kuzidi kuwa Mgumu.

Hivo ni muhimu sana baada ya kupata dalili za gono au kudundulika una ugonjwa wa gono, hakikisha unapata dawa ya Gono ambayo ni sahihi kwa tatizo lako, Usijaribu kila aina ya Dawa.

Hauhitaji Jaribio la kutibu ugonjwa wa Gono – ufuatiliaji wa dawa ya gono au matibabu Sahihi ili kuhakikisha kuwa maambukizi yametibiwa kwa ufanisi – Ni muhimu Zaidi.

Ikiwa dalili za mtu zinaendelea kwa zaidi ya siku chache baada ya kupokea matibabu, anapaswa kurudi kwa mtoa huduma wa afya ili kutathminiwa upya,

Kipimo cha tiba kinahitajika siku 7-14 baada ya matibabu kwa watu wanaotibiwa maambukizi ya koo. Kwa sababu kuambukizwa tena ni kawaida,

wanaume na wanawake walio na ugonjwa wa gono au kisonono wanapaswa kupimwa tena miezi mitatu baada ya matibabu ya maambukizi ya awali, bila kujali kama wanaamini kwamba wenzi wao walitibiwa kwa mafanikio.

Dawa ya gono kwa mwanaume

Kwa Mujibu wa vituo vya kudhibiti na Kuzuia magonjwa “The Centers for diseases control and Prevention- CDC”

Wanashauri kwenye matibabu ya Ugonjwa wa Kisonono au Gono; dawa ya Gono iwe single dose ya Cefriaxone 500mg ambapo ni sindano unachomwa(intramuscular ceftriaxone),

Na Dawa mbadala zingine zinaweza kutumika kama dawa ya Gono endapo dawa ya ceftriaxone haiwezi kutumika.

Ingawa dawa hii itazuia maambukizi ya Gono haitaweza kurudisha madhara yoyote yaliyosababishwa na Ugonjwa huu wa Kisonono au Gono.

Dawa Zingine zinazoweza kutumiwa na wataalamu wa afya kutibu maambukizi ya Neisseria gonorrhoeae bakteria mmojawapo anayeweza kusababisha gono au kwa jina jingine kisonono ni pamoja na;

  • Azithromycin
  • Cefixime
  • Cefotaxime
  • Ceftizome
  • Erythromycin
  • Gemifloxacin
  • Gentamicin

NB: Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya kwa kina kabla ya kutumia dawa yoyote ya Gono ili kupata maelekzo sahihi kulingana na hali yako.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments