Ticker

6/recent/ticker-posts

Hatari ya kimbunga Mauritius yapelekea kufungwa kwa shule



Hatari ya kimbunga Mauritius yapelekea kufungwa kwa shule

Utabiri wa kutokea kwa kimbunga, mvua na mafuriko nchini Mauritius, kumesababisha kufungwa shule ikiwa ni hatua za tahadhari.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji BBC, kisiwa jirani cha Reunion kipo kwenye kiwango cha juu zaidi cha tahadhari ya kimbunga baada ya kukumbwa na kimbunga chenye nguvu kiitwacho Belal.

Mamlaka imeonya wakazi kubaki majumbani na huduma za dharura kukaa tayari kwa ajili ya madhara yanayotarajiwa.

Hali mbaya ya hewa imesababisha vifo katika kisiwa cha Reunion na Mauritius.

Mwili wa mtu ambaye hajajulikana ulipatikana katika kijiji cha cha Saint-Gilles katika pwani ya magharibi ya Reunion muda mfupi kabla ya tahadhari ya kimbunga hicho kutolewa.

Katika kijiji cha Baie-du-Tombeau nchini humo, mzee wa miaka 75 alikufa maji siku ya Jumapili.

Mtu mmoja ameripotiwa kupotea baada ya dhoruba kali baharini huko La Preneuse magharibi mwa Mauritius.



Post a Comment

0 Comments