Kipindupindu Zimbabwe: Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kuanza rasmi
Kipindupindu Zimbabwe: Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kuanza rasmi
Nchini Zimbabwe, serikali inazindua kampeni ya chanjo ya kipindupindu kesho, Jumatatu Januari 29, huku maambukizi yakienea kwa kasi na kuibua wasiwasi nchini humo. Zaidi ya watu 20,000 wameugua katika miezi ya hivi karibuni, na vifo 500 vimerekodiwa.
Wagonjwa wa kwanza wa kipindupindu walirekodiwa nchini Zimbabwe chini ya mwaka mmoja uliopita, kama kilomita mia moja kutoka mji mkuu na, kama kila mwaka, idadi ya kesi huongezeka katika msimu huu wa mvua.
Mwaka huu, anaeleza John Roche, mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kwa kanda ya kusini, janga hilo ni kubwa kuliko kawaida, na maambukizi elfu ya ziada kila wiki, hasa katika maeneo ya mijini.
“Harare imeathirika hasa kwasababu kuna msongamano mkubwa wa watu. Mfumo wa usambazaji maji katika mji mkuu uko katika hali mbaya, ukiwa umetunzwa vibaya kwa miaka kadhaa. Katika baadhi ya vitongoji, hata haipo. Kwa hivyo watu hukimbilia kwenye visima ambavyo maji yake mara nyingi huchafuliwa na vinyesi.
“Hofu yetu leo ni kwamba mwanzoni mwa mwaka watu wanasafiri zaidi, wanarudi kutoka kwenye sherehe za familia vijijini mwao, wengine wamesafiri kwenda nchi za mipakani na shule pia zimeanza tena. Haya yote yanahatarisha kuharakisha kuenea kwa janga hili.
“Kampeni hii ya chanjo ni jambo zuri sana, dozi moja inatoa kinga kwa miezi sita. Kwa bahati mbaya, hakuna chanjo za kutosha na ni vigumu kuzipata. Barani Afrika, tuna magonjwa ya kipindupindu kila wakati. Labda tuanze kufikiria mambo kwa njia tofauti, labda tufikirie juu ya kutengeneza chanjo mashinani,”
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!