kuongezeka uzito kipindi cha ujauzito

kuongezeka uzito kipindi cha ujauzito

Wanawake wengi wakiwa wajawazito lazima waongezeke uzito kati ya kilograms 11.5 mpaka 16 kilograms),

Wengi wao watapata ongezeko la kilogram 1 mpaka 2 kilograms kwenye kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo(First trimester),

Kisha ongezeko la 0.5 kilogram kwa wiki ndani ya kipindi chote cha Ujauzito. Ongezeko la Uzito hutegemea na sababu mbali mbali kipindi cha Ujauzito.

Kumbuka: Mwanamke mwenye Uzito kupita kiasi(Overweight women) anatakiwa kuongezeka chini ya kilogram 4 mpaka 11 kilograms au pungufu ya hapa kutegemea na Uzito aliokuwa nao kabla ya kubeba Ujauzito,

Na Mwanamke mwenye Uzito mdogo(Underweight women) atatakiwa kuongezeka kwa kilogram zaidi ya kilogram 13 mpaka 18 kilograms.

Lakini pia ni lazima uzito wako uongezeke zaidi ikiwa una mtoto zaidi ya mmoja tumboni(multiple pregnancy),

MFANO: kwa Mwanamke mwenye mimba ya mapacha ni lazima aongezeke uzito wa kuanzia kilograms 16.5 mpaka 24.5 kilograms.

Moja ya vitu muhimu vya kuzingatia ili kupata uzito sahihi kwa mjamzito ni lishe, hakikisha unakula mlo kamili wenye virutubisho vyote vinavyotakiwa kwa maendeleo bora ya mtoto au ujauzito wenye afya,

Kwa Wanawake wengi wakiwa wajawazito, hiki ndyo kiwango Sahihi cha kalories wanachotakiwa kupata;

  • 1,800 calories kwa siku kwenye miezi 3 ya kwanza ya Ujauzito(1st trimester)
  • 2,200 calories kwa siku kwenye miezi 3 ya pili ya ujauzito(2nd trimester)
  • 2,400 calories kwa siku kwenye miezi 3 ya tatu ya ujauzito(3rd trimester).

Sababu au Chanzo cha kuongezeka uzito kipindi cha ujauzito

Kwa Aslimia kubwa kuongezeka uzito kipindi cha ujauzito sio kwa sababu ya mafuta kuwa mengi(fat), bali ni sababu zinazohusiana na mtoto,

Na hizi hapa ni sababu kwanini umeongezeka kilogram 16 wakati wa ujauzito;

(1). Mtoto: kuchangia uzito wa kilogram 3.5

(2). Kondo la nyuma(Placenta): kilogram 1 mpaka 1.5 kilograms

(3). Maji ya Uzazi(Amniotic fluid): kilogram 1 mpaka 1.5 kilograms

(4). Tisu za matiti/maziwa(Breast tissue): kilogram 1 mpaka 1.5 kilograms

(5) Ugavi wa damu(Blood supply): kilograms 2

(6) Mafuta/Fat stores: kilogram 2.5  mpaka 4 kilograms

(7). Ongezeko la kizazi(Uterus growth): kilogram 1 mpaka 2.5 kilograms.

Jinsi ya kudhibiti kuongezeka uzito kipindi cha ujauzito

Ni muhimu kujua jinsi ya kudhibiti Uzito ukiwa mjamzito ili kukusaidia kuwa na ujauzito wenye afya bora na kujifungua Salama.

Wanawake wengine tayari wana uzito kupita kiasi kabla hata ya kupata ujauzito. Wengine huongezeka uzito haraka sana wakati wa ujauzito. Kwa njia yoyote, mwanamke mjamzito anapaswa kuongezeka uzito kwa kiwango kinachotakiwa wakati wa ujauzito kulingana na umri wa mimba yake.

Ni bora kuzingatia kula vyakula sahihi na kufanya Mazoezi. Ikiwa hutapata uzito wa kutosha wakati wa ujauzito, wewe na mtoto wako mnaweza kuwa na matatizo.

Hivi hapa ni baadhi ya Vidokezo vinavyoweza kukusaidia kudhibiti kuongezeka uzito kipindi cha ujauzito;

✓ Kula Mlo kamili wenye virutubisho vinavyotakiwa kwa kiwango sahihi,

Usisahau matunda na mboga za majani kwa wingi kwenye mlo wako, vitu hivi vina vitamins vya kutosha na kiwango kidogo cha Calories na mafuta(fat).

✓ Epuka vyakula au vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha Sukari

✓ Usile vyakula vya mafuta mengi kwa kiwango kikubwa, kama vile Chips n.k

✓ Hakikisha unafanya Mazoezi,

Unashauriwa kufanya mazoezi kwa kiasi(Moderate exercise), kwa ajili ya afya yako na mtoto aliyetumboni,

Hii husaidia pia kuunguza kalories zilizozidi.

Mazoezi kama vile; Kutembea na kuogelea ni mazoezi mazuri kwa mama mjamzito.

Hakikisha Unazungumza na mtoa huduma wako kabla ya kuanza programu ya mazoezi.

Hivyo ndyo baadhi ya vidokezo kuhusu kuongezeka uzito kipindi cha ujauzito.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!