kusinzia baada ya kula,chanzo na jinsi ya kuzuia hali hii

kusinzia baada ya kula,chanzo na jinsi ya kuzuia hali hii

Hali ya kusinzia baada ya kula chakula kwa kitaalam hujulikana kama “Postprandial somnolence”

kusinzia baada ya kula ni hali ambayo huwatokea watu wengi na huweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo; Wingi wa chakula ulichokula, Muda uliokula chakula chako n.k

Vyakula vyenye mafuta mengi pamoja na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Wanga(High-fat and high-carbohydrate foods) vimeonekana kuchangia uwepo wa hali hii ya kusinzia baada ya kula,

Pia hali ya afya yako kwa ujumla pamoja na muda wako wa kulala,vyote hivi huweza kuchangia kuhisi uchovu sana na kusinzia baada ya kula.

Fahamu kwamba; Kufanya uchaguzi sahihi wa vyakula, kiwango, pamoja na muda wa kula huweza kusaidia kuepuka hali ya uchovu sana pamoja na kusinzia baada ya kula.

Hali hii ya kusinzia baada ya kula sio tatizo kubwa la kukufanya uwe na wasi wasi, labda kama linaathiri shughuli zako za kila siku, masomo yako au maisha yako kwa ujumla,

Kwa baadhi ya Cases, Hali hii huleta matokeo mabaya kwenye utendaji kazi na uzalishaji eneo la kazi na hata kuongeza hatari ya kupata Ajali mbali mbali zikiwemo ajali za magari n.k.

Watafiti hawana uhakika kabisa kwa nini ni kawaida kwa watu kupata usingizi baada ya kula. Uchunguzi unaonyesha kuwa kiwango kikubwa cha nishati(Energy level) baada ya kula huweza kuwa chanzo,

Mlo mkubwa unaweza kusababisha usingizi, na muundo wa chakula unaweza kuwa na athari pia. Utafiti umegundua kuwa milo iliyo na mafuta mengi, wanga, au kalori inaweza kuongeza usingizi.

Inaweza kuwa vigumu kutambua sababu ya moja kwa moja ya wewe kupata usingizi baada ya kula. Badala yake, kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kusinzia baada ya kula, na sababu hizo zinaweza kubadilika kulingana na mtu na mlo wake anaokula.

Vyakula vinavyosababisha Kusinzia baada ya kula

Vyakula vinavyoweza kusababisha kusinzia baada ya kula ni vipi?

Utafiti zaidi unahitajika ili kuelewa jinsi virutubisho na vyakula tofauti huathiri matukio ya usingizi wa mchana. Zaidi ya hayo, tafiti nyingi kuhusu chakula na usingizi huzingatia usingizi wa usiku, ambao ni tofauti na kuelezea kuhusu nishati ya mchana. Hata hivyo, baadhi ya aina za vyakula huenda zikasababisha usingizi.

Hivi hapa ni baadhi ya vyakula vinavyoweza kuongeza hatari ya mtu kupata hali ya kusinzia baada ya kula;

1. Vyakula vya mafuta mengi(High-fat foods)

Vyakula vya aina hii vinaweza kuwa vigumu kumeng’enywa na kuongeza uwezekano wa mtu kupata uchovu baada ya kula(post-meal tiredness) pamoja na kupata hali ya kusinzia baada ya kula.

2. Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha wanga(High-carbohydrate)

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kula chakula chenye kiwango kikubwa cha wanga huongeza uwezekano wa kusinzia baada ya kula.

3. Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Tryptophan(protein-amino acid),

Tryptophan ni amino acid ambayo hujulikana kwa kuhamasisha mchakato wa usingizi ndani ya ubongo,

Vyakula vyenye aina hii ya amino acid ni pamoja na; ndizi,shayiri pamoja na  chocolate.

Ingawa tryptophan pekee haiwezi kusababisha usingizi kila wakati, athari zake huimarishwa inapoliwa na wanga.

4. Vyakula jamii ya karanga

Vyakula hivi vina kiwango kikubwa cha melatonin ambayo huhusika moja kwa moja na swala la Usingizi.

Ingawa vyakula hivi vinaweza kusababisha usingizi wa baada ya kula, si kila mtu atapata uchovu baada ya kuvila kwani mambo mbalimbali huathiri jinsi mwili unavyoitikia mlo.

Summary;

Swala la kupata Usingizi baada ya kula huweza kutegemea;

– Aina ya Kile unachokula; Mfano; kula vyakula vyenye mafuta mengi,kiasi kikubwa cha Wanga n.k

Aina ya virutubisho unavyopata mfano; tryptophan, melatonin na vingine.

– Kiasi unachokula; Kula chakula kingi,chenye kiwango kikubwa cha Calories ukiwa umekaa sehemu moja huweza kupelekea wewe kusinzia baada tu ya kula.

– Muda unaokula chakula; pia Swala la muda uliokula chakula huweza kuwa chanzo cha Usingizi baada ya kula.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!