Mabilionea 5 Ulimwenguni waongeza utajiri wao mara mbili Zaidi Tangu mwaka 2020.
#Wakati mabilionea wakiongeza utajiri, kwa upande mwingine watu karibu bilioni tano walikuwa masikini zaidi katika kipindi hicho.
Inaelezwa kuwa mabilionea hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla Elon Musk, Bernard Arnault na familia yake ya kampuni ya kifahari ya LVMH, mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, mwanzilishi wa Oracle Larry Ellison na gwiji wa uwekezaji Warren Buffett – utajiri wao uliongezeka kwa asilimia 114 mnamo 2020 wakati dunia ikipambana na janga la Uviko.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la Oxfam, utajiri wa mabilionea hao uliongezeka kutoka dola bilioni 405 mwaka 2020 na kufikia dola bilioni 869 mwaka jana. Kwa hivi sasa utajiri wao umefikia Dola trillioni 3.3, licha ya mizozo mingi ya ulimwengu iliyoyumbisha uchumi wa dunia.
📷: Bilionea Jeff Bezos na Elon Musk.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!