Mama Maria Nyerere atimiza umri wa miaka 93

Mama Maria Nyerere atimiza umri wa miaka 93.

MTANDAO: RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuungana pamoja kumuombea na kumtakika heri, mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mama Maria Nyerere.

Rais kupitia mitandao yake ya kijamii siku ya Desemba 31, 2023 aliandika Mama yetu wa Taifa, Mama Maria Nyerere leo anatimiza umri wa miaka 93.

“Tuungane pamoja kuendelea kumuombea afya njema, furaha, amani, na wakati mwema katika kumbukumbu hii muhimu kwenye maisha yake.” Ameandika Rais Samia.

Mama Maria, amehudumu Ikulu kama Mke wa Rais wa Tanzania, kuanzia mwaka 1964 hadi 1985, wakati Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere alipoamua kung’atuka.

Kuanzia Disemba 1962 hadi Aprili 1964, Mama Maria amehudumu kama Mke wa Rais wa Tanganyika.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!