MAMBO MUHIMU YA KUFANYA KWA MTU ANAYEHARISHA NA KUTAPIKA.
✅Haraka sana tumia mchanganyiko wa maji ya chumvi na sukari(ORS)
✅Kama huna ORS kunywa maji kwa wingi.
✅Nenda haraka Kituo cha huduma za afya huku ukinywa maji safi na salama kwa wingi
JE, UNAWEZAJE KUJIKINGA NA MAGONJWA YA KUHARISHA NA KUTAPIKA?
✅Kunywa maji yaliyochemshwa au kutibiwa na dawa ya Klorini.
✅Nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kabla ya kula au kumlisha mtoto.
✅Nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni baada ya kutoka chooni.
✅Tumia choo kwa usahihi kila wakati na tupa kinyesi cha mtoto kwenye tundu la choo
#elimu_ya_afya
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!