Mchungaji ampika mboga Muumini wake ili asichepuke

Mchungaji ampika mboga Muumini wake ili asichepuke

Mchungaji mmoja nchini Zambia, ameushangaza umma baada ya kumpika mmoja wa washirika wake wa kiume wakati wa ibada ili aweze kubadilika nankuwa mume mwema.

Kitendo hicho kilitokana na Mwanaume huyo kudaiwa kwenda nje ya ndoa na kilisababisha kuwekwa kwa kikao cha usuluhishi na ushauri, huku Mchungaji huyo akiamua kulipeleka suala hilo kwenye ulimwengu wa kiroho.

Mara baada ya maombi, Mchungaji huyo alidai Mungu alimwambia ampike kwenye sufuria mwanaume huyo mbele ya madhabahu, ili aache michezo ya kuchepuka na iwe fundisho kwa wengine.

Inaarifiwa Mwanaume huyo, alitii na alionekana akiwa ndani ya Sufuria kubwa na mchungaji akiwa amesimama karibu yake akimkoroga bila kujua hatma baada ya pishi hilo.

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo pia alikuwa akiweka mchanganyiko wa Vitunguu, Pilipili na Nyanya kwenye sufuria hilo, ili kufanikisha zoezi huku waumini wengine wakishuhudia tukio hilo.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!