Mshtuko wa moyo baada ya Mbwa kutafuna $4,000 kwenye kabati

Mbwa atafuna $4,000 kwenye kabati la jikoni.

Cecil, mbwa kutoka Pennsylvania, amekuwa maarufu baada ya kutafuna bahasha ya pesa ambayo wamiliki wake walikuwa wametenga kwa ajili ya kumlipa mkandarasi wao pesa taslimu kwa ajili ya kuweka uzio.

Mapema Desemba, Clayton Law aliweka bahasha iliyokuwa na $4,000 kwenye kabati lake jikoni kwake huko Pittsburgh, Pennsylvania.

Baadaye, kwa mshangao, walimkuta mbwa wao kipenzi akifurahia mlo wa thamani zaidi maishani mwake, akiacha vipande vichafu vya pesa vilivyotawanyika kila mahali.

“Ghafla Clayton alifoka kwa sauti, ‘Cecil anakula $4,000!'” Carrie Law alisema “Nilifikiri, ‘Sijasikia vizuri.’ Nilisogea na kupata mshtuko wa moyo.”

Wanandoa hao walianza zoezi ambalo hawakulitarajia na la kuchosha: Kuunganisha pamoja noti zao na kutafuta nambari za noti ili kupewa noti mpya na benki kama mbadala.

Je Angekuwa mbwa wako ungefanya nini?

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!