Mtoto wa Mr.Ibu aiba Michango ya Matibabu ya baba yake.
Polisi nchini Nigeria wamemkamata mtoto wa kiume na mtoto wa kike wa kuasili wa mwigizaji maarufu wa vichekesho nchini Nigeria John Okafor, maarufu Mr Ibu, kutokana na madai ya kuiba pesa zilizokusudiwa kwa matibabu ya mwigizaji huyo.
Onyeabuchi Okafo na Jasmine Okekeagwu wanadaiwa “kumiliki simu ya mwigizaji huyo na kuingia katika mfumo wa benki”, kabla ya kuiba Naira milioni 55 sawa na dola $60,700.
Pesa hizo ni sehemu ya fedha ambazo zilikuwa zikichangwa na mashabiki na watu wenye mapenzi mema kwa ajili ya matibabu ya mwigizaji huyo, baada ya kuugua kwa muda mrefu mwaka jana.
Ugonjwa huo ulisababisha kukatwa kwa mguu mmoja wa Okafor.
Via:bbcswahili
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!