Mwanaume miaka 54 kutaka kumuoa binti wa miaka 4

Hasira zimezuka nchini Nigeria baada ya mwanamume wa miaka 54, ‘kumuoa’ msichana wa miaka minne ili ‘kuokoa maisha yake.

Wazazi wa msichana huyo, mzee wa miaka 54, kiongozi wa kimila na wengine walioshiriki katika ndoa hiyo, walifikishwa mbele ya jopo la Serikali ya Bayelsa kujielezea baada ya malalamiko ya watu.

Walieleza kuwa ndoa kati ya ‘bibi harusi’ huyo wa miaka minne na mwanaume huyo ni ibada ya kitamaduni inayoitwa ‘Koripamo’ ya kuokoa maisha ya mtoto huyo.

Baba wa mtoto huyo alisema binti yake alikuwa akiumwa sana kila mara na kueleza kuwa kwa mujibu wa mila za Akedei njia pekee ya kuokoa maisha yake ni mwanaume kulipa mfano wa mahari.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!