Weka maji yako kwenye chombo kisafi chenye mfuniko.
Zingatia:maji yakiwa ya tope yachujwe kwanza na kitambaa kisafi kisha yawekwe kwenye chombo chenye mfuniko.
✅Weka kidonge kimoja cha Klorini katika ujazo wa lita 10 za maji au vidonge viwili kwenye ujazo wa lita 20 za maji na kisha funika na tikisa ili ichanganye vizuri.
✅Subiri kwa muda wa dakika 30 na baada ya muda huo unaruhusiwa kunywa maji hayo.
✅Maji yako ya kunywa sasa ni salama .
TAHADHARI:
✅Usimeze kidonge cha Klorini.
✅Vidonge vya Klorini viwekwe mbali na watoto pamoja na mwanga wa jua.
✅Maji ya kunywa yahifadhiwe vizuri na epuka kuchota kwa kutumbukiza kikombe au kata kwa usalama zaidi chombo kitakachotumika kuhifadhia kiwe na koki kuwezesha uchotaji wa maji hayo kwa urahisi.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!