Rekodi ya Mbwa Mzee Zaidi Duniani kuchunguzwa.
Mbwa wa Ureno aitwaye Bobi aligonga vichwa vya habari mwaka jana alipotawazwa kuwa mbwa mzee zaidi kuwahi kutokea duniani na Guinness World Records (GWR) – akiipiku rekodi ya awali iliyodumu kwa karne moja.
Bobi alifariki mwezi Oktoba akiwa na umri rasmi wa miaka 31 na siku 165.
Lakini sasa rekodi yake hiyo imetiliwa shaka, baada ya baadhi ya madaktari wa mifugo kutilia shaka ushahidi wa umri wa Bobi.
Bobi alikuwa mbwa wa aina ya Rafeiro do Alentejo ambao wana wastani wa kuishi miaka 12 hadi 14.
Maafisa wa Rekodi ya dunia ya Guiness (GWR) sasa wamesitisha taji hilo na kuanzisha uchunguzi upya.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!