Sababu na jinsi ya kuzuia kukakamaa kwa Joints

Hali ya joints kukakamaa baada ya kupumzika inaweza kuonekana kawaida, lakini kukakamaa kwa muda mrefu inaweza kuwa shida katika afya yako. Hali ya kukakamaa kwa joints inaweza kutokea baada ya kutazama sana vipindi vya runinga,kukaa sehemu moja kwa muda mrefu,kukaa kwenye gari wakati wa safari ndefu n.k

Kwa hivyo, kwa nini joints zako hukakamaa baada ya kunyeshewa na mvua kubwa? Na kuna wakati ambapo hisia hiyo ni ishara ya wasiwasi mkubwa zaidi? zifuatazo ni sababu za hali hiyo

Ni nini husababisha ukakamavu wa joints wakati wa asubuhi?

Viungo(joints) vinahitaji lubrication ili kufanya kazi vizuri. Ndio maana unapaka mafuta ili kulainisha. kwa mfano ni kama vile kupaka bawaba ya mlango mafuta ili isipige kelele.

Joints(Viungo) vyako huwa vinakuwa na kilainishi asilia kinachojulikana kitaalamu kama synovial fluid. Kiowevu (synovial fluid) hiki cha mnato hujaza nafasi ya kukutana kati ya mifupa na mfupa mwingine. Kiowevu hiki jinsi kinavyoteleza huruhusu harakati laini ndani ya magoti yako, viwiko na viungo vingine.

Kadiri unavyosogea, ndivyo umajimaji huu unavyozidi kuzunguka kwenye viungo vyako ili kuweka kila kitu kiteleze.

Lakini unapopumzika, lubricant hiyo inakaa na kutulia bila mzunguko wowote wa utelezi ndani ya joints. Hivyo kupelekea baadhi ya viungo kukakamaa.

Jinsi ya kuzuia viungo/Joints kukakamaa.

Ushauri bora hapa unafaa karibu kila suala la afya. “Ni muhimu sana kufuata mtindo wa maisha mzuri,” “Unaweza kupunguza matatizo mengi kwenye viungo vyako ikiwa:

  • utafanya checkup ya uzito wako mara kwa mara.
  • kufanya mazoezi mara kwa mara.
  • kula lishe bora.
  • kupunguza msongo wa mawazo na kupumzika ipasavyo.”
  • Kutokukaa sehemu moja kwa muda mrefu.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!